top of page
Abstract Background
Search

Balozi Dkt. Elsie S. Kanza Afanya Ziara Dallas, Texas

  • Writer: Leo Nzali
    Leo Nzali
  • Mar 8
  • 1 min read

Updated: Mar 13



Katika ziara hiyo, Balozi Kanza alizindua rasmi Nevet Counseling Center, kituo cha ushauri na tiba ya afya ya akili kilichopo ndani ya jengo la Holy Cross Lutheran Church. Kituo hicho kinamilikiwa na Deborah Mwamgomo LPC-A na kinalenga kutoa huduma za ushauri wa afya ya akili kwa Watanzania na jamii pana ya Waafrika wanaoishi Texas.


Akizungumza na The Diaspora Magazine, Bi. Mwamgomo alisema kituo hicho kitasaidia kukabiliana na changamoto za maisha ya ughaibuni kwa kutoa ushauri wa kitaalamu unaozingatia pia mila na utamaduni wa Kitanzania.


Balozi Dkt. S. Kanza akiwasili katika ofisi za Nevet Counseling Center(kusho), Pastor Dkt. Absalom nasuwa,(kulia) Deborah Mwangomo, LPC-A
Balozi Dkt. S. Kanza akiwasili katika ofisi za Nevet Counseling Center(kusho), Pastor Dkt. Absalom nasuwa,(kulia) Deborah Mwangomo, LPC-A

Katika hafla hiyo pia, Balozi Dkt. Kanza alisaini kitabu kipya cha Mental Health and Parenting in Diaspora kilichoandikwa na Deborah Mwamgomo, kinachozungumzia afya ya akili na malezi kwa familia zinazoishi nje ya nchi(ughaibuni).


Aidha, Balozi Kanza alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la 12 la Umoja International Prayerline na alipata fursa ya kukutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi Dallas kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu huduma za ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. 🇹🇿


Balozi Dkt. S. Kanza akipokea kitabu cha "Mental health and Parenting in diaspora" kutoka kwa mtaalamu na mshauri wa afya ya akili Bi. Deborah Mwangomo, LPC-A
Balozi Dkt. S. Kanza akipokea kitabu cha "Mental health and Parenting in diaspora" kutoka kwa mtaalamu na mshauri wa afya ya akili Bi. Deborah Mwangomo, LPC-A



 
 
 

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
Nala get $10.png
137092063_4184719214890090_5004613881637175391_n.0.jpeg
social media flyer copy.png
NZALI.jpg

Leo Nzali (nzalinextlevel)

Journalist, Producer and Graphics Designer of this magazine The Diaspora also DallasGospel magazine..
Keep following our pages for more information about the diaspora

Let the posts come to you.

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter
  • Pinterest

Call 

214-971-0534 

Email 

Follow

  • Facebook
  • Twitter
  • LinkedIn
  • Instagram
bottom of page