top of page
Abstract Background
Search

Balozi Dkt. Kanza Ahamasisha Diaspora Kuwekeza Tanzania

  • Writer: Leo Nzali
    Leo Nzali
  • Mar 11
  • 2 min read

Updated: Mar 13


Matukio haya yamejiri mwishoni mwa wiki hii jijini Dallas, Texas, katika maadhimisho ya miaka 12 tangu kuanzishwa kwa huduma ya Umoja Prayerline huduma ya maombi kwa njia ya mtandao inayofanyika kwa lugha ya Kiswahili na kuwakutanisha Watanzania na waumini mbalimbali wanaoishi ughaibuni.


Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Elsie S. Kanza. Akitoa hotuba yake, Mheshimiwa Balozi alitoa wito kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi kuendelea kuwekeza nyumbani Tanzania ili kuchangia maendeleo ya taifa.


“Ningependa kutoa rai kwa wana Diaspora kuendelea kuwekeza nyumbani Tanzania. Serikali ya Tanzania inatambua nafasi muhimu inayochezwa na Watanzania wa diaspora katika maendeleo ya taifa letu. Kupitia uwekezaji mnaoufanya nyumbani kwa njia mbalimbali, mmekuwa chombo muhimu katika kuleta fursa kwa taifa letu, ikiwemo katika biashara, ajira, elimu pamoja na sekta nyingine nyingi zinazowanufaisha Watanzania,” alisema.


Mh. Balozi Dkt. Kanza katika picha ya pamoja na mchungaji kiongozi wa makanisa ya umoja Pastor Dkt. Absalom Nasuwa
Mh. Balozi Dkt. Kanza katika picha ya pamoja na mchungaji kiongozi wa makanisa ya umoja Pastor Dkt. Absalom Nasuwa

Aliongeza kuwa Serikali inaendelea kuthamini mchango huo na kuahidi kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani utaendelea kutoa ushirikiano na msaada kwa Watanzania wa diaspora katika maeneo mbalimbali yanayoweza kuchangia maendeleo ya nchi. Katika hotuba yake, Balozi Kanza pia alisisitiza umuhimu wa amani, uhuru wa kuabudu na uhuru wa kujieleza katika jamii. Alieleza kuwa misingi hiyo imekuwa muhimu katika kudumisha mshikamano na utulivu nchini Tanzania.

Alibainisha kuwa serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, imeweka kipaumbele katika kuhakikisha uhuru wa kuabudu na kudumisha amani nchini, huku taasisi mbalimbali zikiendelea kushirikiana katika kuimarisha misingi hiyo.

Kwa upande mwingine, Ubalozi wa Tanzania uliipongeza Kanisa la Umoja kwa mchango wake wa kuwaunganisha Watanzania wanaoishi ughaibuni kutoka makundi na maeneo mbalimbali kupitia huduma za kiroho na kijamii.


Pichani Kulia ni Director Umoja Prayerline Dada Jessica Katalahiya katika picha ya kumbukumbu na Balozi Dkt. E. S. Kanza
Pichani Kulia ni Director Umoja Prayerline Dada Jessica Katalahiya katika picha ya kumbukumbu na Balozi Dkt. E. S. Kanza

Aidha, Balozi Kanza aliwahimiza Watanzania wa diaspora kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa dira ya maendeleo ya taifa, Tanzania Development Vision 2050, ambayo inalenga kuelekeza maendeleo ya Tanzania katika kipindi cha miaka 25 ijayo. Alisisitiza kuwa ushiriki wa diaspora katika uwekezaji, biashara, elimu, mafunzo na ushirikiano wa kimataifa utaendelea kuwa nyenzo muhimu katika kuharakisha maendeleo na ustawi wa taifa la Tanzania pamoja na wananchi wake.


 
 
 

Comments

Rated 0 out of 5 stars.
No ratings yet

Add a rating
Nala get $10.png
137092063_4184719214890090_5004613881637175391_n.0.jpeg
social media flyer copy.png
NZALI.jpg

Leo Nzali (nzalinextlevel)

Journalist, Producer and Graphics Designer of this magazine The Diaspora also DallasGospel magazine..
Keep following our pages for more information about the diaspora

Let the posts come to you.

  • Facebook
  • Instagram
  • Twitter
  • Pinterest

Call 

214-971-0534 

Email 

Follow

  • Facebook
  • Twitter
  • LinkedIn
  • Instagram
bottom of page